WAKALA WA TAIFA WA UTAFITI
utafiti wa Nyuntba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA)
1.0 Utangulizi:
Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi ulianzishwa kwa sheria ya Wakala wa Serikali Na.30 ya mwaka 1997 kulingana na mageuzi ya mfumo wa utendaji kazi kiufanisi Serikalini.
Makao Makuu ya Wakala, Mwenge , Dar es salaam
Madhumuni ya NHBRA
Madhumuni ya NHBRA ni kuwawezesha wananchi wa Tanzania kufanikiwa kupata nyumba bora kwa kutumia rasilimali zipatikanazo hapa nchini na ufundi mahsusi ifikapo mwaka 2025.
Majukumu ya NHBRA
Kutoa huduma za utafiti na vifaa bora kuhusiana na nyumba za gharama nafuu kwa lengo la kuinua kiwango cha ubora wa nyumba za kuishi na hivyo kuinua maisha ya watu wa mijini na vijijini kwa ujumla.
NHBRA inatoa na kusambaza teknolojia ya vifaa bora vya ujenzi.na ufundi ili:-
- Kupata nyumba imara
- Kupata nyumba safi kwa afya ya binadamu.
- Kupata nyumba zenye ubora unaozingatia mila, desturi na heshima ya binadamu.
Muundo wa NHBRA
NHBRA iko chini ya Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Wizara inasaidiwa na Bodi ya Ushauri (Ministerial Advisory Board) chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu. Wakala unaendesha shughuli zake za kila siku chini ya uongozi wa Mtendaji Mkuu (Chief Executive)
Semina ya Uhamasishaji zinazoendeshwa na Wakala kuhusu Ujenzi wa Nyumba bora naUtengenezaji wa Vifaavya Ujenzi
NHBRA ina Idara kuu tatu:-
- Idara ya Utafiti na Maendeleo (Research & Development)
- Idara ya Ushauri wa kitaalamu (Consultancy
- Idara ya Utawala na Biashara. (Business Support)
Kazi za NHBRA
Kulingana na Sheria ya Wakala wa Serikali No.30 ya mwaka 1997. mhimili wa kazi za NHBRA umeanishwa ndani ya Muundo wake hapo juu. Kazi za NHBRA zinajumuisha huduma na vifaa kama ifuatavyo:-
(a) Huduma zitolewazo:
- Kuendesha utafiti wa vifaa bora na ufundi na ujenzi kwa lengo la kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba.
- Kuuza matokeo ya utafiti wa kitaalamu.
- Kutoa huduma ya ushauri, usanifu, ukadiriaji gharama na usimamizi wa ujenzi wa nyumba.
- Kuendesha mafunzo na semina mbalimbali kuhusu nyumba za gharama nafuu zitumiazo maliasili ya eneo la ujenzi.
- Kuendesha utafiti wa kijamii na kiuchumi hususani makazi ya binadamu.
- Kupima ubora wa vifaa vya ujenzi na ubora wa majengo ndani ya maabara na kwenye maeneo ya ujenzi.
- Kutoa huduma za uchoraji na ukataji wa vyuma,mbao,vigae na vifaa vingine ndani ya karakana zake.
- Huduma za ujenzi, ukarabati na matengenezo ya nyumba.
- Kutoa huduma ya maktaba maalum ya maendeleo ya nyumba bora.
- Kuishauri Wizara mama juu ya sera ya Nyumba Bora na makazi ya Binadamu.
(b) Baadhi ya vifaa vipatikanavyo NHBRA
- Mashine za kufyatua matofali yanayofungamana (interlocking)
- Mashine za kawaida za kufyatua matofali.
- Mashine za kutengeneza vigae bora vya kuezeka nyumba.
- Kalibu mbalimbali za vigae na matofali
- Matofali yanayofungamana.
- Matofali yaVyoo bora vya VIP.
- Samani bora za nyumbani.
- Madawati bora ya bustanini.
- Madawati bora ya shule za msingi na sekondari.
- Majalida, ripoti za utafiti,
- Miongozo ya kiufundi na vipeperushi.
- Ramani za nyumba bora.
NHBRA iko wapi?
NHBRA iko barabara ya Sam Nujoma umbali wa mita 400 kutoka barabara ya All Hassani Mwingi kuelekea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, karibu na kituo cha mabasi cha Mwenge Wilayani Kinondoni.

Maabara ya kupima ubora wa vifaa vya ujenzi
Mikakati ya NHBRA
NBHRA inaweza na iko tayari kushirikiana na jumuiya mbalimbali za kijamii (CBOs), Mashirika,yasiyo ya kiserikali (NGOs) ,Vyama vya ushirika n.k. Wizara, Idara na Wakala za serikali.Wafadhili na Watu binafsi katika kutekeleza majukumu yake. Huduma na ufuatiliaji wa karibu unaotolewa kuhakikisha kuwa huduma bora zinapatikana wakati wote.
Ili NHBRA ifanikiwe katika huduma zake ni muhimu kuwa:
- Matokeo ya utafiti juu ya makazi ya binadamu yanapatikana kulingana na mahitaji ya wateja kwa muda unaotakiwa.
- Asilimia kubwa ya nyumba mpya zinazojengwa katika maeneo yaliyohamasishwa na NHBRA ziwe zimetumia utaalamu wa NHBRA.
- Huduma bora za utafiti na ushauri zinatolewa.
- Huduma na vifaa bora za vya kitaalamu ili kuwaridhisha washiriki na wadau vinatolewa.
- Mapato ya wakala yanaongezeka
Mbinu za kusambaza matokeo ya utafiti na utaalamu
NHBRA imeandaa mikakati ya utekelezaji wa majukumu yake (Strategic Plan) kutokana na mchanganuo wa kibiashara (Business Analysis) kwa lengo la kutoa huduma safi na bora.
- Huduma mbalimbali na utaalamu vinarahisishwa na kupatikana kirahisi kutokana na:
- Utafiti na kutembelea wadau, washitiri na wateja ili kuharakisha mahitaji yao.
- Matangazo na makala katika vyombo vya habari.
- Utafiti wa masoko map/a. Kushiriki maonyesho mbalimbali ya biashara.
- Mbinu shirikishi za mafunzo kwa vitendo.
- Machapisho mbalimbali Kushiriki mikutano, warsha, semina na kongamano mbalimbali za kitaalamu.
- Kukaribisha wanafunzi wa vyuo kwa mafunzo ya vitendo (Practical Training)
- Wakala umeshaanza kuunda na kutoa mafunzo kwa vikundi vya ujenzi (Grassroot Building Brigades-GBBs) ngazi za vijii, kata.Tarafa naWilaya vitakavyohusika na uzalishaji wa vifaa na ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika maeneo yao. Vikundi hivi vitapewa mbinu za kujiendesha kibiashara ili kukuza ajira hasa kwa vijana.
- Pia NBHRA imeanza kuingia mikataba ya maelewano (Memorandum of Understanding and Service Level Agreements) na watu binafsi, makampuni na taasisi, mashika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na jumuiya za kijamii (CBOs) za kitaifa na kimataifa kwa ajili ya kutangaza na kusambaza teknolojia ya nyumba bora za gharama nafuu nchini kama mchango wa kuondoa umaskini katika jamii ya Tanzania.
Maombi yote yapelekwe kwa:
Mtendaji Mkuu
S.LP 1964,DARES SALAAM
Simu 255 022 2771971
255 022 2774003
Fax: 255 022 2774003
Mob: 2550754210270