News

October 29th, 2012
Picha ni, Mh. Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka akimkabidhi Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete anwani ya Ofis
September 21st, 2012
Includes new regions and districts
September 11th, 2012
FINANCIAL YEAR: 2012/2013

Extra Menu

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Submitted by ardhi on Mon, 08/13/2012 - 10:08
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tarehe 7Agosti 2012, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi, Mheshimiwa Prof. Anna K. Tibaijuka (MB), aliongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwasilisha Ombi la Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, mjini New York linaloelezea kwa kina matokeo ya kisayansi na kiufundi yanayothibitisha madai ya Tanzania ya eneo la ziada nje ya ukanda wa kiuchumi baharini.
Ujumbe wa Tanzania ulijumuisha Mhe. Ramadhan Abdullah Shaaban, Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati kutoka Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar; Mhe. Mgeni Hassan Juma Relly, Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar; Mhe. James Daudi Lembeli (MB), Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Mazingira; na Bw. Patrick Rutabanzibwa, Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Mradi wa Kudai Eneo la Ziada baharini. Aidha, Ujumbe ulijumuisha timu ya wataalam iliyoongozwa na Prof. Evelyne Mbede wa Idara ya Jiolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamisheni ya mipaka Baharini Prof. Lawrence Folajimi Awosika wa Nigeria, amesifu wasilisho la kina na ufasaha la Tanzania, na kutokuwepo kwa migogoro ya mipaka ya bahari na jirani zake Kenya na Shelisheli ambazo Tanzania ina makubaliano ya mipaka ya bahari na nchi hizo.
Tarehe 30 Septemba 1985, Tanzania iliridhia Mkataba wa Sheria ya Bahari ya Umoja wa Mataifa (United Nations Convention on the Law of the Sea (UNCLOS)) ya mwaka 1982 na kuwa moja ya nchi wa wanachama wa Mkataba huo, mwaka 1994. Kwa mujibu wa Ibara ya 76 ya Sheria ya Bahari, nchi zote zinazopakana na Bahari na zilizoridhia Sheria ya Bahari kabla ya tarehe 13 Mei, 1999 zilitakiwa kuwasilisha maombi yenye taarifa za kisayansi na kiufundi kabla ya tarehe 13 Mei, 2009 kwa ajili ya kupata stahili ya kumiliki eneo la ziada mbele ya maili 200 za bahari nje ya Ukanda wa Kiuchumi baharini. Hata hivyo, kutokana na uhaba wa taarifa za kisayansi na ufundi, Tanzania iliwasilisha Andiko la awali mnamo tarehe 7 Mei, 2009 kama ilivyokubalika na nchi zilizoridhia Sheria ya Bahari katika mkutano wa mwezi Juni, 2008. Tanzania iliwasilisha Andiko Kamili kwenye Umoja wa Mataifa tarehe 8 Januari, 2012.
Umoja wa Mataifa uliialika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda kutoa maelezo ya kisayansi na kiufundi kuhusu Andiko la Tanzania mbele ya Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Mipaka ya Bahari katika kikao chake cha thelathini kilichopangwa kufanyika kuanzia tarehe 30 Julai hadi tarehe 10 Agosti, 2012. Andiko lilitoa mchanganuo wa taarifa za kisayansi na kiufundi ikiwa ni pamoja na ramani kulingana na taratibu chini ya Ibara ya 76 (Continental Shelf) ya Sheria ya Bahari.
Kufuatia wasilisho hilo, Umoja wa Mataifa itatafakari na kutoa mapendekezo juu ya Andiko la Tanzania kwa mujibu wa Kanuni za Taratibu za Kamisheni.
Katibu Mkuu
10 Agosti, 2012

PreviewAttachmentSize
Press Release KISWAHILI.pdf23.91 KB