News

May 8th, 2012
Application Form
April 16th, 2012
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi yasherehekea miaka 50 ya Uhuru
April 12th, 2012
Mhe. Prof. Anna Tibaijuka (Mgeni rasmi ) katika sherehe hizo

Extra Menu

Operesheni ya Kukomesha Vurugu Mijini

Submitted by alexkaraba on Fri, 09/09/2011 - 15:41
Operation Restore Urban Order

 

 

 Prof. Anna Tibaijuka akizungumzanawaandishi wa habari, Dar es Salaam janakuhusu uvamizi wa ardhi na mabadiliko holela ya matumizi ya ardhi katika miji mbalimbali nchini. Kushoto ni Naibu wake, Bw. Goodluck Ole Medeye. 08.09.2011

 

Operesheni ya Kukomesha Vurugu Mijini

1.  Miji yetu hapa nchini ambayo kwa sasa ni Halmashauri za Jiji 4, Manispaa 17 na miji midogo 90 huendelezwa kwa kufuata Mipango ya Jumla(General Planning Schemes) kama Mipango Kabambe na Mipango ya Muda(Master Plans and Interim Land Use Plans), na Mipango ya Kina(Detailed Schemes/Layouts). Mipango Kabambe ipo 21, Mipango ya muda ni 29 na Mipango ya kina ni 5,000.

 2. Kwa mujibu wa sheria za nchi, mtu yeyote haruhusiwi kufanya maendelezo yoyote mjini bila kibali cha maandishi kutoka kwenye mamlaka za upangaji (Planning Authorites), ambazo ni Halmashauri za Jiji, Manispaa, Miji na Wilaya chini ya usimamizi wa Wizara/Waziri mwenye dhamana ya Mipango miji (kwa wakati huu ni Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi). Kwa hiyo Planning Authorities zikikiuka misingi hii Waziri ana mamlaka ya kutengua maamuzi hayo. 

 3. Kutokana na maendeleo kijamii, kiuchumi, kitamaduni, kisiasa, na kimazingira, mipango ya maendeleo ya miji siyo ‘static’. Kuna wakati mipango ya matumizi ya ardhi hupitwa na wakati, na hivyo kulazimika kubadilishwa/kuhuishwa (Redevelopment Schemes). 

 4.  Hata hivyo, ni vizuri ieleweke kuwa ubadilishaji wa matumizi ya ardhi haufanyiki kiholela bali kwa Sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa. Pia mipango ya matumizi ya ardhi nayo haifanyiki kiholela bali huandaliwa kwa kuzingatia sera, sheria na kanuni, hivyo ubadilishaji lazima uzingatie taratibu hizo.

 5. Sheria zinazohusika na ubadilishaji wa matumizi ya ardhi ni za Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 kifungu cha 35, na Mipango miji namba 8 ya mwaka 2007 vifungu vya 30-32. Lipo pia Tangazo la Serikali namba 678 la mwaka 1964 linalohusu marekebisho ya mipango(modification of schemes)

 6. Aidha, zipo nyaraka za kitaalam (technical circulars) zilizoandaliwa ili kutoa miongozo ya kutekeleza sheria hizo. Nyaraka hizo ni namba 1 wa mwaka 1995 na namba 1 wa mwaka 2006.

 7. Wizara imekuwa ikitoa matamko kwa umma kuhusu uvamizi wa maeneo ya wazi likiwemo la tarehe 29/12/2010 lililowataka wananchi kutoa taarifa kila wanapoona uvamizi ukifanyika kwenye maeneo ya wazi.

 8.Wizara pia kupitia barua yake yenye kumb.na. CB 437/502/01/98 ya tarehe 27 Julai 2011 imezielekeza Mamlaka zote za Upangaji (Serikali za mitaa) kuandaa mipango pale ambapo haipo, na kuhuisha mipango iliyopitwa na wakati.

 9. Tarehe 29 Agosti 2011, Wizara kupitia barua yenye kumb.na. CB.437/502/01/107 imeziagiza Mamlaka za upangaji ‘Kuondoa matumizi ya ardhi yasiyo halali, yanayokinzana na kuleta kero kwa wananchi’. Haya nipamoja na gereji, vilabu vya pombe, kumbi za starehe n.k.

 10. Hatua za kubadili matumizi ya ardhi zilizoainishwa kwenye sera, sheria, kanuni na miongozo ni:

·        Maombi kupokelewa na mamlaka ya upangaji.

·        Bango kuandaliwa na kuwekwa kwenye eneo husika kwa  siku 30.

·        Maombi kujadiliwa na kamati inayohusika na maendeleo ya miji.

·        Maamuzi ya kamati kupelekwa Wizara ya Ardhi kwa uamuzi. Hatua hii imekuwa ikikiukwa na kusababisha migongano isiyo ya lazima.

 11. Kumekuwa na ubadilishaji wa matumizi ya ardhi kiholela yakiwemo maeneo ya wazi na yale ya umma yaliyotengwa kwa matumizi ya huduma za jamii; kwa mfano, hivi karibuni eneo la mabwawa ya maji taka Mikocheni limevamiwa na kupimwa viwanja 12(namba 1116-1127). Viwanja hivyo ni batili na hivyo vimefutwa.

 Mabadiliko yote ya ardhi ambayo yamefanyika bila kufuata utaratibu ni batili na yanatakiwa yaondolewe mara moja. Tunaweka msisitizo kwamba wananchi wawe macho wasitapeliwe na maafisa wasio waadilifu maana hawa wanawahadaa tu. Hati miliki zote zilizotolewa kinyume cha Sheria na taratibu zitafutwa (with immediate effect) kama ilivyofanyika Ocean Road, Palm beach, Jangwani beach na Mbezi beach.

 12. Chini ya kamati ya uchunguzi iliyoundwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa William Lukuvi, maeneo ya wazi yapatayo 153 yaliyopo katika Halmashauri za Manispaa zote tatu za Mkoa wa Dar es Salaam yalichunguzwa. Kutokana na uchunguzi huo ilibainika kwamba:-

 ·        Maeneo 88 (sawa na asilimia 80) kati ya maeneo 110 ya wazi yaliyopo katika Manispaa ya Kinondoni yamevamiwa.

 ·        Katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala maeneo ya wazi yaliyokaguliwa ni 30, na kati ya hayo maeneo 11 yamevamiwa. Hii ni sawa na asilimia 37 ya maeneo yote yaliyokaguliwa na Kamati.

·        Kwa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, imeonekana kuwa na asilimia ndogo ya uvamizi, ambapo yalibainika maeneo 5 sawa na asilimia 30 ya maeneo ya wazi yaliyotembelewa ambayo ni 14.