Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bibi Maria H. Bilia kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Bibi Bilia anakuwa ni miongoni mwa manaibu Makatibu Wakuu tisa (9) walioteuliwa kuongoza Wizara mbalimabli.
Taarifa iliyotolewa Jumanne tarehe 20 Julai, 2010 Jijini Dares Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon Luhanjo inaonyesha kuwa uteuzi wa Naibu Makatibu Wakuu hao unaanzia tarehe 15 Julai, 2010 na wataapishwa rasmi siku ya Alhamisi tarehe29 Julai, 2010 saa 4.00 asubuhi.
Kabla ya uteuzi huo, Bibi Bilia alikuwa ni Katibu Tawala (RAS) wa Mkoa wa Kagera. Aidha, aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kabla ya kuwa RAS mwaka 2008.
Manaibu Makatibu wakuu wengine nane walioteuliwa ni pamoja na Bwana Ngosi C.X. Mwihava (Ofisi ya Makamu wa Rais.), Balozi Herbert E. Mrango (Wizara ya Miundombinu) Balozi Rajab Gamaha ambaye (Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa) na Bwana Mbogo Futakamba ( Wizara ya Maji na Umwagiliaji).
Wengine ni Dk. Yohana L. Budeba (Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi), na Bibi Maria H. Bilia ambaye ni Katibu Tawala waMkoa wa Kagera kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Aidha, Rais Kikwete amewateua Bibi Nuru H.M. Mlao (Wizara ya Maliasili na Utalii) Bwana Hussein A. Katanga (Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto) na Bwana Job D.Masima (Wizara ya Ulinzina Jeshi la Kujenga Taifa)