News

August 4th, 2010
Ardhi Institutes
July 21st, 2010
YAPATA NAIBU KATIBU MKUU
July 12th, 2010
nyumba na maendeleo ya makazi
May 24th, 2010
REGISTRATION OF TOWN PLANNERS
April 23rd, 2010
DESEMBA 2005 HADI DESEMBA 2009
April 23rd, 2010
Kigamboni New City Master plan
March 25th, 2010
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Extra Menu

Utoaji wa Hatimiliki za Kimila

Submitted by ardhi on Fri, 04/02/2010 - 23:49
Utoaji wa Hatimiliki za Kimila

 “ Kuanza utekelezaji wa Mkakati wa Kurasimisha Rasimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) kwa lengo la kuwawezesha watanzania kurasimisha Ardhi na Nyumba zao ili waweze kuzitumia kupata mikopo kutoka kwenye mabenki na mifuko mingine ya fedha inayokopesha.......” Kwa wale wenye mawazo kwamba Ilani ya Uchaguzi ya CCM haitekelezeki, basi mradi huu ni jibu kamili kwao.

Utaratibu wa kupima mashamba na kutoa hatimiliki za kimila kwa wakulima wa wafugaji umeanza katika baadhi ya Wilaya kama vile; Mbozi, Iringa, Handeni, Bagamoyo, Kilindi, Kisarawe na Monduli, lakini katika Wilaya hizo utaekelezaji ulifanywa katika baadhi ya Vijiji na kwa baadhi tu ya wakazi wa Vijiji hivyo kwa kadri ya wale waliotaka mashamba yao yapimwe. Mradi tunaouzindua leo utekelezaji wake ni tofauti kwa kuwa utahusisha Vijiji vyote Wilayani na mashamba yote ndani ya Vijiji husika. Mradi huu kwa hiyo ni wa kwanza wa aina yake hapa nchini na unaofanywa kwa majaribio katika Wilaya mbili za Bariadi na Babati. Baada ya hapo utasambazwa ufike katika Wilaya zote nchini. Wilaya hizi mbili (za Bariadi na Babati) zimeteuliwa kwa kigezo cha kuwakilisha Wilaya zenye mchanganyiko sawia baina ya wakulima na wafugaji. Katika Wilaya hii ya Bariadi, tutaanza utekelezaji kwa majaribio katika Vijiji 9 ambavyo ni: Mwakibuga, Old Maswa, Bupandagila, Nakabindi, Sanungu, Nyaumata, Nyangokolwa, Ngwanagwali na Bahemuhi.

Uzoefu na mafunzo yatakayopatikana katika upimaji wa mashamba na maeneo ya malisho katika vijiji hivi tisa utasaidia kurahisisha kazi hii katika Vijiji vilivyobakia. Lengo ni kutekeleza mradi huu katika Vijiji vyote Wilayani hapa. Kazi itakayofanyika kwanza ni kutambua matumizi ya ardhi katika kila kijiji, yaani eneo la Makazi, Huduma za kijamii kama Shule, Zahanati, Majengo ya ibada, Makaburi, Hifadhi ya ardhi ya kijiji, eneo la malisho ya mifugo n.k. Wataalam toka Tume ya Matumizi Bora ya Ardhi watasaidia kufanikisha kazi hii ya kupanga matumizi bora ya ardhi kwa kila Kijiji.

Baada ya kutambua kila kipande cha ardhi ndani ya kijiji na matumizi yake, ndipo utekelezaji utafanywa wa kutambua mipaka ya kila mwenye shamba au eneo la malisho ya mifugo na kuweka mipaka, aidha itafunguliwa rejesta/daftari la kuweka kumbukumbu za miliki ya ardhi ya kila mwanakijiji na kisha kumpatia kila mhusika hatimiliki ya eneo lake. Kipande cha ardhi cha shamba au malisho kinaweza kumilikishwa kwa mtu mmoja mmoja, au familia ya mume na mke au kama eneo linamilikiwa kiukoo, basi hati itatolewa kwa ukoo husika kupitia kwa kiongozi wa ukoo. Ili kazi hii ifanyike kwa haki na kwa mafanikio, ni lazima kila mwanakijiji ashirikishwe. Kimsingi huu ni mradi shirikishi. Kwa mfano shamba la mtu linapopimwa ni lazima kwanza serikali ya kijiji kupitia kamati ya Ardhi ya Kijiji ithibitishe kwamba kweli muhusika ndiye mwenye shamba hilo au eneo hilo la malisho; na kwamba halina mgogoro. Pili Kazi ya kutambua mipaka ya shamba hilo ni lazima ithibitishwe na majirani zake wote wanaozunguka shamba hilo, hivyo ni lazima wawepo ili wathibitishe na wakubaliane juu ya mipaka yao na huyo anayepimiwa eneo lake. Mfano huu natoa ili kuonyesha umuhimu wa wanajamii kushirikishwa katika kila hatua ya mradi huu. Hivyo elimu kwa umma ni suala muhimu kabisa ili mradi huu ueleweke na uungwe mkono na wana vijiji wote. Mradi huu utatekelezwa chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Wilaya na Serikari za Vijiji, Aidha vitaundwa vikosi kazi ambavyo vitashirikisha wana kijiji wenyewe pamoja na wataalamu watakaoongoza kazi .

Kazi ya kutoa Elimu kwa umma kuhusu mradi huu ilianza tarehe 10/02/2009 kule Dodoma ambapo Wizara yangu ilikutana na kamati ya Wabunge inayosimamia masuala ya Ardhi, pia walishiriki na Viongozi wakuu wa Mkoa na Wilaya yenu. Katika kikao hicho Wizara yangu ilitoa maelezo kuhusu mradi huu, na leo ni hatua ya pili ambapo Wizara yangu imekutana na viongozi wengi zaidi wa ngazi ya Wilaya na Kata, na wachache kutoka Vijiji vitakavyohusika na mradi huu. Hatua ya tatu elimu kuhusu mradi itafikishwa hadi kwa Viongozi na Wanavijiji katika Vijiji vyao. Mhe. Mkuu wa Mkoa. Ili kufanikisha mradi huu, ni muhimu katika ngazi ya Wilaya na Vijiji viwepo vyumba maalum vya kutunza nakala za hatimiliki za wanavijiji kwa lugha ya kitaalam vyumba hivi huitwa masjala. Pili katika ofisi za Halmashauri sharti ziwe na masjala ya kutunza kumbukumbu zote za miliki ya kila kipande cha ardhi, ramani za mashamba, ramani za mipaka ya vijiji n.k. Hali kadhalika katika jengo la ofisi ya Kijiji kitengwe chumba cha Masjala. Chumba hiki yawekwe makabati imara ya kutunza nakala za hatimiliki za kila mwanakijiji. Hati hizo zina thamani kama fedha, hivyo lazima zituzwe vizuri ili zisingie vumbi, zisinyeshewe mvua, zisiliwe na mchwa wala panya n.k.

Vile vile chumba hiki kiwe na milango na madirisha imara ili kulinda hati zisiibiwe kirahisi. Hapa nasisitiza umuhimu wa kuanzishwa masjala za umiliki wa ardhi. Mhe. Mkuu wa Mkoa, Naomba nimalizie salamu zangu za kuzindua mradi huu kwa kueleza umuhimu wa wakulima kupimiwa maeneo na kupewa hatimiliki kama ifuatavyo; Kwanza ni lazima tuelewe kwamba duniani kote mtu anaye miliki ardhi, anamiliki utajiri lakini hapa nchini pamoja na wananchi wengi waishio vijiji kuwa na ardhi bado ni maskini. Sababu kubwa ni kwamba ardhi yao haijapimwa na kumilikishwa kisheria. Hivyo basi ili ardhi iwe mtaji hai, ni lazima ipimwe na kumilikishwa na anayemiliki atambulike kisheria. Pili anayemiliki ardhi akishatambuliwa rasmi kisheria kwa kupewa hatimiliki, anaweza kutumia hatimiliki hiyo kama dhamana ya kupata mikopo benki ili kujipatia mtaji wa maendeleo. Hivyo wananchi wa Bariadi ambao hawakopesheki kwenye mabenki kwa kukosa dhamana, sasa baada ya kupewa hatimiliki watakuwa wanakopesheka, hivyo huu ni ukombozi mkubwa kiuchumi na ni silaha muhimu ya kupiga vita umaskini.