News

October 29th, 2012
Picha ni, Mh. Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka akimkabidhi Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete anwani ya Ofis
September 21st, 2012
Includes new regions and districts
September 11th, 2012
FINANCIAL YEAR: 2012/2013

Extra Menu

Huduma za Upimaji Ramani

 

HUDUMA YA UPIMAII RAMANI
Majukumu ya Idara kwa Ujumla

Majukumu ya Idara
Upimaji na Ramani ni Idara katika Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi. Jukumu lake kubwa ni usimamizi wa upimaji ardhi na utayarishaji wa ramani na plani mbalimbali za nchi mijini na vijijini. Ramani hizo ni msingi wa kubuni, kutekeleza na kuratibu mipango ya maendeleo juu ya ardhi katika sekta na kwa matumizi mbalimbali kama:
  • Umilikishaji ardhi
  • Kupanga matumizi ya ardhi
  • Utalii
  • Mawasiliano
  • Makazi
  • Kilimo
  • Hifadhi ya mazingira
  • Utafiti na uchimbaji madini

2.   Bidhaa zinazouzwa

Urasimu ramani

2.1   Ramani.
Ramani   za   msingi   kutokana   na picha za anga (base maps):
  • Ramani za topografia za skeli ya kati 1:50,000 kwa nchi nzima  
  • Ramani za maeneo ya mijini katika skeli ya 1:2,500 au 1:5,000
Ramani za kuzalisha kutokana na ramani za msingi  
  • Ramani katika skeli ya1:250,000 
  • Ramani za Mikoa na Wilaya katika skeli kati ya 1:300,000 -1:500,000
  •           Ramani za masomo maalum
  • Ramani ya Barabara ya Tanzania katika skeli 1:2m 
  • Ramani yaTawala za Mikoa na Wilaya katika skeli ya l:2m 
  • Ramani ya Jiji la Dar es Salaam katika skeli ya I :20,000 
  • Ramani ya Utalii ya Mlima Kilimanjarokatikaskeli ya 1:1 00,000
2.2 Picha za Anga
Idara ya upimaji na ramani ina maktaba ya picha za anga za sehemu mbalimbali za nchi zilizopigwa katika       nyakati mbalimbali tangu miaka ya 1940. 
  • Picha za ,skeli ndogo chini ya 1:50,000
  • Picha za skeli ya kati I :20,000   1:50,000
  • Picha za skeli kubwa zaidi ya 1:20,000
2.3 Takwimu na kumbukumbu za
Upimaji Ardhi.
Idara ni mhazini wa takwimu na kumbukumbu   za   upimaji   miliki nchini
  • Kadi za vielelezo vya alama za msingi za upimaji 
  • Vipimo vya alama za msingi za upimaji
  • Plani za upimaji miliki
2.4 Bidhaa Maalum
Idara    ina    uwezo    kivifaa    na kitaaluma   kutayarisha   ramani, na kutoa huduma mbalimbali kukidhi mahitaji ya wateja
  • Ramani maalum, kulingana na ubunifu na vigezo vya mteja
  • Picha-ramani (orthophoto)
  • Muunganisho wa picha nyingi kuwa moja.
  • Ramani katika mfumo wa kompyuta
  • Ramani ya awali iliyochorwa kwa mashine za photogrammetry  Kumbukumbu Kuu ya Uoto kwa nchi nzima(katika mfumo wa kompyuta)
  • Picha za anga katika mfumo wa kompyuta kwa baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam
3.0 Huduma Mbalimbali
3.1   Upimaji
Idara    ina    uwezo    kivifaa    na kitaaluma kufanya upimaji wa aina mbalimbali
  • Upimaji miliki ukubwa wowote mahali popote nchini
  • Upimaji wa kuweka mifumo ya alama za msingi za upimaji
  • Upimaji kwa ajili ya utayarishaji wa ramani kutokana na picha za anga
  • Upimaji kwa kazi za uhandisi kama vile:
  • Miinuko na ubapa wa barabara 
  • Mapito ya njia za mawasiliano
3.2 Uchoraji na Uchapaji wa
Ramani
  • Tafsiri na utambuzi wa alama katika picha kwa madhumuni ya kuchora ramani, matumizi ya ardhi ama uoto juu-yake.
  • Uchoraji kwa mitambo ya photogrammetry
  • Usanifu wa ramani
  • Utoaji nakala za ramani au plani katika filamu kwa kamera maalum
  • Ukuzaji wa nyaraka kwa njia ya kamera hadi x6
  • Kushona vitabu
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Uchapaji ramani
  • Kuchapa ramani katika rangi nyingi au moja hadi ukubwa wa 30" X 40"
3.3 Uwezo wa Kupima na Kuchora Ramani kwa Teknolojia ya Kompyuta.
  • Uchoraji wa ramani kwa kutumia mashine za photogmmmetry zilizoshikizwa na kompyuta
  • Uingizaji wa ramani katika kompyuta kwa njia ya board or screen digitization hadi ukubwa wa AO 
  • Upimaji ardhi kwa kutumia kifaa cha Total Station ambacho hunasa vipimo na takwimu moja kwa moja katika mfumo wa kompyuta 
  • Upimaji kwa taaluma ya anga za juu GPS
  • Kupata ramani ya umbile la ardhi kuonyesha mwinuko na mabonde usawa wa bahari
  • Upimaji wa mwinuko wa barabara
  • Usanifu wa ramani kwa kompyuta


UCHORAJI RAMANI KUTOKANA NA PICHA ZA ANGA

  • Kuchapa ramani kutoka kwenye kompyuta katika rangi moja au nyingi
4.    Teknolojia ya Kisasa
Kwa kutumia teknolojia ya kisasa, idara ina uwezo wa kuchora na kutoa ramani katika mfumo wa kompyuta. Ramani za baadhi ya maeneo hususan ya kati ya Jiji na Manispaa zote nchini ziko katika mfumo wa kompyuta. Ramani au Kumbukumbu Kuu ya Uoto wa Tanzania ipo katika mfumo wa kompyuta
5.    Upatikanaji wa Bidhaa na Huduma za Idara.
5.1   Huduma za Upimaji na
Ramani
Bidhaa za kawaida zikiwemo ramani, picha za anga huuzwa katika duka la ramani lililopo jengo la Casino katika makutano ya barabara za Kivukoni Front na Luthuli, jijini Dar es Salaam
5.2 Bidhaa na huduma ya pekee hupatikana kwa maombi ya mteja.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:
Mkurugenzi,
Idara ya Upimaji na Ramani
S.L.B. 9201, Dares Salaam
Simu: 255-22-2121894/2123735
Fax: 2138962/2123735
barua kipepe: smd@raha.com

Upimaji Miliki
1.0 Utangulizi
Lengo la upimaji wa ardhi ni kupata kielelezo halisi na cha kipekee cha utambulisho wa kipande cha ardhi hususan sehemu kilipo, umbile na ukubwa wake na uhusiano na mazingira yanayokizunguka. Hi mwananchi aweze kupewa hati ya kumiliki ardhi hakuna budi kuwa na kumbukumbu ya mipaka ya kipande cha ardhi husika. Upimaji wenye lengo hilo huitwa upimaji miliki (cadastral survey)
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Ramani inayoonyesha viwanja baada ya upimaji kukamilika
2.0 Upimaji Miliki Mijini:
Maombi   ya   miliki yanawasilishwa kwa Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya, Jiji, Manispaa au Mji husika. Afisa   Ardhi atakagua eneo kuthibitisha kuwa:
  • Ardhi husika ina mchoro wa mipangomji ulioidhishwa
  • Ardhi husika ni huru, haina migogoro ya mipaka, miliki au hati iliyowekwa rehani
  •  Ardhi husika haina upimaji uliotangulia na kama upo haikusudiwi kuutumia kumilikisha ardhi hiyo. Afisa ardhi atafanya mawasiliano na Mpima    ardhi    wa    Halmashauri husika kwa kujaza fomu SF     37 (request for survey) ikiambanishwa na     mchoro     wa     mipangomiji ulioidhinishwa.    Mpima Ardhi wa Halmashauri atatoa maelekezo ya Upimaji   (Survey Instruction)   kwa mpimaji.
Baada ya upimaji kukamilika, nyaraka zote za upimaji huwasilishwa kwa Mkurugenzi wa upimaji na Ramani kukaguliwa, kuthibitishwa na kusajiliwa kama kumbukumbu rasmi ya mipaka ya Ardhi husika.
Upimaji mijini huzingatia michoro ya Mipango miji na sio mipaka ya asili jinsi majirani wanavyokaa. Hapa ndipo umuhimu wa kuwa na ardhi huru unapojitokeza ili yeyote anayeathiriwa na utekelezaji wa mchoro wa mipango miji ashirikishwe kikamilifu ikiwa ni pamoja na kufidiwa kwa mujibu wa sheria.
Chini ya Sheria Sura Na. 390 (Sheria ya Upimaji Ardhi) plani ya upimaji iliyoidhinishwa ndio uthibitisho rasmi wa mipakaya ardhi iliyopimwa. Kutokana na hili hatua ya kuomba upimaji, utekelezaji wake, ukaguzi, uthibitishwaji na usajili wa plani lazima viwe makini kuepusha matatizo kama vile miliki kutolewa juu ya nyingine.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Upimaji wa ardhi kwa kutumia vifaa vya mawasiliano
ya masafa ya anga za juu (Satellite Global Positioning
System)
3.0 Upimaji Miliki Kijijini:
Maombi ya upimaji ardhi yanawasilishwa kwa Afisa Ardhi wa Halmashauri. Afisa Ardhi atachunguza na kuthibitisha yafuatayo:
  • Ardhi iliyoombewa upimaji ni ya mhusika na kuwa ni huru na haina migogoro ya miliki au mipaka.
  •  Iwapo mhusika ni mwekezaji, kijiji kimetenga ardhi hiyo ili ihawilishwe kumilikishwa na kamishna wa ardhi.
  • Kuna mihutasari ya vikao vya Halmashauri ya kijii vilivyopitisha / vilivyotenga Ardhi kwa mwekezaji.
  • Vibali vya kumiliki ardhi kulingana na ukubwa wake vinapatikana katika ngazi ya Kijiji, Wilaya, Mkoa au Wizara.
Afisa Ardhi atawasiliana na Mpima wa Halmashauri kwa kujaza fomu SF 37 (Request for Survey) iliyoambatana na mchoro wa ardhi inayoombewa upimaji, nakala za mihutasari na vibari vya kumilikisha.
Upimaji unapokamilika, nyaraka zote huwasilishwa kwa Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kukaguliwa, kuthibitishwa na hatimaye kusajiliwa kama kumbukumbu rasmi ya mipaka ya ardhi iliyopimwa. Plani za hati (deed plan) huandaliwa kutokana na Plani za upimaji zilizothibitishwa.
Kwa maoni au maswali wasiliana na:
Mkurugenzi, Upimaji na Ramani
P.O. Box 9201,
Simu: +255-22-21373513894
Fax: +255-22-21237335138962
Kivukoni/Luthuli Road
Email:smd@raha.com
Tovuti: www.ardhi.go.tz