News

October 29th, 2012
Picha ni, Mh. Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka akimkabidhi Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete anwani ya Ofis
September 21st, 2012
Includes new regions and districts
September 11th, 2012
FINANCIAL YEAR: 2012/2013

Extra Menu

Huduma za Maendeleo ya Makazi

 

HUDUMA YA MAENDELEO YA MAKAZI

 

Majukumu ya Idara kwa Ujumla
1.0 Uendelezaji wa Makazi Nchini
 
Uendelezaji wa makazi nchini unaongozwa na Sera ya Makazi yaTaifa pamoja na Sheria ya Mipango Miji Sura ya 378 ya mwaka 1956 iliyorekebishwa mwaka 1961. Kwa miongozo hiyo, shughuli zote za uendelezaji   wa        makazi zinasimamiwa na Halmashauri husika za Wilaya, Miji, Manispaa na Jiji kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana ya Maendeleo ya Makazi.
 
2.0 Majukumu ya Wizara kuhusu uendelezaji wa Makazi
  • Kuandaa Sera na sheria/kanuni za kuendeleza makazi na kusimamia utekelezaji wake.
  • Kuandaa mipango ya kimbinu ya kuendeleza miji (Strategic Urban Development plans)
  • Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Nyumba.
  • Kusimamia mfuko wa Mikopo kwaWatumishi wa Serikali (Revolving Housing Loan Fund).
  • Kuandaa mipango ya kuendeleza maeneo ya kati ya miji na kuidhinisha michoro ya makazi.

.

 

 2.1 Kubuni Michoro ya Makazi

Michoro ya maeneo ya Makazi huandaliwa na Halmashauri husika na huidhinishwa na Wizara.Wizara hushiriki katika maandalizi pale tu ambapo Halmashauri itakapoomba msaada wa wataalam wa kusaidia katika utekelezaji wa jukumu hilo. Utaratibu ufuatao hutumiwa na halmashauri katika kuandaa michoro hiyo
  • Kutambua eneo na kulitangaza kwenye gazeti la Serikali.
  • Kuwajulisha wananchi walio ndani ya eneo lililotambuliwa
  • Kufanya uthamini wa maendelezo ndani ya eneo na kulipa fidia.
  • Kubuni michoro ya makazi na matumizi ya ardhi na kuiwasilisha kwenye Kamati ya Mipangomiji na Mazingira ili ijadiliwe.
  • Baada ya michoro kupitishwa na Kamati, huwasilishwa kwa Waziri mwenye dhamana ya maendeleo ya makazi ili iidhinishwe.
  • Mchoro ukishaidhinishwa hurudishwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya utekelezaji.

 

2.2      Kuandaa Mipango ya Kimbinu ya Kuendeleza Miji (Strategic Urban Development Plans)
Maandalizi ya Mipango hii hufanywa na   Halmashauri   husika   za   Miji, Wilaya,   Manispaa   na Jiji. Wizara hushiriki kwa kutoa utaalam pale inapoombwa na Halmashauri hizo. Maandalizi ya Mipango hii hufuata utaratibu ufuatao:
  •  Uhamasishaji wa madiwani, watendaji na watoa huduma muhimu za kijamii, kiuchumi na kitaasisi.
  •   Maandalizi ya rasimu ya mpango wa mazingira.
  •  Mkutano Mkuu wa majadiliano/mashauriano na wadau wote.
  •  Uainishaji wa masuala muhimu ya kijamii na kiuchumi yanayohusu maendeleo ya eneo.
  •  Kuunda vikundi kazi kushughulikia na kuchambua masuala muhimu.
  • Kubuni mbinu za kimkakati za kushughulikia masuala yote muhimu yaliyoainishwa.
  • Kuandaa mpango wa utekelezaji wa mikakati iliyobuniwa.
  • Kuandaa mpango endelevu wa mji pamoja na michoro husika
  • Kuwasilisha mpango kwa wadau kwa maafikiano.
  • Kuwasilisha mpango kwa halmashauri husika.
  • Mpango kuidhinishwa na Waziri mwenye dhamana ya kuendeleza makazi

  •  Mpango ulioidhinishwa hurudishwa kwenye Halmashauri kwa utekelezaji.
  • Usimamiaji wa mpango ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa utekelezaji na kufanya mahuisho
2.3 Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Nyumba
Uendelezaji wa nyumba kwa kiasi kikubwa hufanywa na wananchi wenyewe. Serikali ina jukumu la kuweka mazingira yatakayosaidia katika uendelezaji huo. Jukumu kubwa ni kuandaa Sera husika na kusimamia utekelezaji wake. Katika maandalizi ya Sera hiyo yafuatayo ambayo huchangia katika uendelezaji wa nyumba huzingatiwa..
  •  Upatikanaji wa viwanja vya kujenga
  •  Upatikanaji wa vifaa vya ujenzi
  • Kuwepo kwa vyombo vya kukopesha kwa ajili ya ujenziwa nyumba na hudumazinazohusika.
  • Ufundi wa ujenzi na viwanda vya kuzalisha vifaa vya ujenzi.
  • Teknolojia ya ujenzi
  •  Kuwepo kwa vyama vya ushirika kwa ujenzi wanyumba
  •  Sheria na kanuni zinazohusu uendelezaji wa nyumba.
  • Ushirikishwaji wa Sekta binafsi katika uendelezaji wa nyumba. 
2.4 Kusimamia/kuthibiti uendelezaji wa makazi
Katika eneo hili Wizara hutekeleza yafuatayo:
  • Kutafiti na kutangaza viwango vya mahitaji ya ardhi kwa matumizi mbalimbali
  •  Kutangaza maeneo yaliyoiva kuendelezwa kimji baada ya kujadiliana na Halmashauri husika.
  • Kuidhinisha/kukataa maombi ya kubadili matumizi ya ardhi yaliyowasilishwa kutoka kwenye Halmashauri.
  •  Kuandaa kanuni mbalimbali za uendelezaji wa Makazi kufuatana na Sheria ya Mipango Miji Sura 378 ya mwaka 1956 iliyorekebishwa mwaka 1961.
  • Kutangaza maeneo wazi na maeneo yanayofaa kwa shughuli za kitalii kwa ajili ya kuhifadhiwa.

 

2.5       Huduma ya Mikopo ya Nyumba kwa Watumishi wa Serikali
Wizara ya Ardhi husimamia mfuko wa Mikopo ya Nyumba kwa Watumishi wa Serikali. Mikopo hutolewa kwa ajili ya kujenga nyumba mpya.kukarabati nyumba, kukamilisha ujenzi wa nyumba, au kununua nyumba. Mkopo huo hutolewa kwa kuzingatia masharti yafuatayo:-
  • Mwombaji hujaza fomu ya maombi na kuipitisha kwa mwajiri wake ikiwa na viambatanisho vifuatavyo:
  • Kivuli cha Hati Miliki ya kiwanja anapokusudia kujenga nyumba. Mchoro wa jengo.
  •  Makisio ya gharama za ujenzi (B/lls  of Quantities)
  • Kibali cha ujenzi toka Halmashauri ya Wilaya/ Mji/ Manispaa/ Jiji husika.
  •  Salary Slip
Sekretariat ya Mfuko iliyopo Wizara ya ardhi inapokea, inachambua maombi na kuyawasilisha kwenye Bodi ya Mfuko ili kutolewa uamuzi. Wale wote walioidhinishiwa mikopo kwa kuzingatia fedha zilizoko kwenye
Mfuko wanaandikiwa kufahamishwa.
  • Mwombaji akikubali mkopo, anatayarishiwa na kutumiwa mkataba wa mkopo anaotakiwa kusaini na kushuhudiwa na Hakimu Mkazi jaji au Wakili.
  • Mhusika kutuma mkataba uliosainiwa pamoja na Hati miliki ya kiwanja ili Wizara nayo isaini mkataba huo.
  • Mhusika kulipia gharama zote za kuweka rehani Hati Miliki na za kusajili mkataba kwa msajili wa Hati.
  • Malipo ya mkopo kwa awamu huanza kutolewa baada ya usajli wa Hati miliki na rehani kukamilika.
  • Mkopaji kuanza kurejesha mkopo kwa kukatwa mshahara wake baada ya mwaka mmoja tangu kupewa malipo ya kwanza ya mkopo.
  •  Mkopaji kurejesha mkopo kwa muda usiozidi miaka 30 kutegemea na muda uliokubaliwa na pande zote mbili na kutajwa kwenye mkataba.
  •  Mikopo hutozwa riba ya asilimia 3 kwa mwaka.
Kwa maoni au maswali wasiliana na: Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo
ya Makazi
S.LP.2067I   Dar es Salaam,
Simu:2l2l034/2l2l24l/9
 
Telephone +255 22 2113165/ 2121241-9 Extension 2434
+255 22 2118303

PreviewAttachmentSize
mipango1.JPG37.17 KB
mipango2.JPG13.95 KB
mipango3.JPG19.48 KB
mipango4.JPG15.18 KB